Vigezo na Masharti

1 UTANGULIZI

Karibu kwenye "Lugha Zetu" (www.lughazetu.com), huduma ya kujifunza na kuzungumza lugha kwa njia ya mtandao inayoendeshwa na Kampuni ya Research and Development Network Limited (RDN). Huduma hii inakuwezesha kuzungumza lugha za Makabila yaTanzania, Afrika na lugha za Kimataifa. Lengo kuu la huduma hii ni kutoa jukwaa linalokuwezesha kujifunza lugha mbalimbali za makabila ya Tanzania, na lugha nyingine ya Kiafrika na za Kimataifa kwa urahisi na kwa haraka. Huduma hii pia imetengenezwa ili kuhifadhi lugha za makabila kama urithi. Huduma hii pia inatoa fursa kwa kizazi cha vijana walioko mjini kujifunza kwa urahisi. lugha za makabila. Jumla ya lugha za makabila 156 ya Tanzania, zaidi ya lugha 2,144 za makabila ya Kiafrika na lugha kubwa za Kimataifa zimeunganishwa na mfumo wetu ili uweze kuongea popote pale.

 

2. MATUMIZI YA TOVUTI

 

2.1 MAUDHUI

Unakubaliana kutoa,taarifa sahihi, ambayo haikiuki hakimiliki, alama za biashara, haki ya faragha na haki ya kutangaza.  Endapo utakiuka, unakubali kuwajibika.

 

2.2 FARAGHA

Taarifa zako za zitalindwa na Sera ya Faragha ya Lugha Zetu wakati wa kutumia huduma hii. Ni jukumu lako kusoma, kuelewa na kuzingatia Sera ya Faragha ya Lugha Zetu.

 

2.3 HAKI MILIKI

Ni jukumu lako na unakubaliana kuheshimu Haki Miliki na Lebo za Biashara za Lugha Zetu and za watu wengine unapotumia tovuti hii. Ni jukumu lako kutujulisha ikiwa kuna ukiukaji wowote wa hakimiliki yako.

 

2.4 MWINGILIANO NA TOVUTI ZINGINE

Lugha Zetu haiwezi kuchunguza maudhui yote yanayohusishwa kutoka kwenye tovuti nyingine kwenye sehemu yoyote ya tovuti hii. Lugha Zetu haidhibitishi upatikanaji wa tovuti hizo. Unakubali kwamba Lugha Zetu haitakuwa na jukumu au haitahusika kwa madhara yoyote yanayosababishwa na matumizi ya maudhui yoyote kutoka tovuti zilizounganza na Lugha zetu. Soma masharti ya tovuti hizo kabla haujatumia.

 

2.6 MGOGORO

Ikiwa kuna mgogoro wowote kuhusiana na matumizi ya tovuti kati ya watumiaji na sisi. Unakubali kutatua mgogoro huo kwa imani nzuri. Ikiwa mazungumzo yameshindwa, ni wajibu wako kufungua mzozo wowote au madai yanayohusiana na matumizi yako ya tovuti yetu. Unakubali kwamba RDN au Lugha zetu pamoja na Mawakala wake walioidhinishwa hawatakuwajibika na uharibifu wowote kama matokeo ya migogoro kati ya watumiaji wa tovuti

 

2.7 KINGA

Tumejitolea kukupa huduma bora, salama na ya kuaminika lakini hatuwezi kuthibitisha kuwa inaweza kuwa haina hitilafu kwa sababu ya mambo yalioko zaidi au chini ya uwezo wetu. Kwa hiyo, kwa kiwango kamili kinachokubalika na Sheria, RDN / Lugha Zetu, wafanyakazi / mfanyakazi na washirika wake kupewa kinga ya kutokuwajibishwa.

 

2.8 FIDIA

Unakubaliana kuidhinisha RDN / Lugha Zetu, wakurugenzi wake, maafisa, wafanyakazi, na ushirikiano wake dhidi ya yoyote au matendo, madeni, madhara, madai au mahitaji ambayo yanajumuisha lakini hayakuwepo kwa ada za kisheria na gharama za ada za kisheria zinazotokea wewe au mtu mwingine wakati wa kutumia huduma tovuti au uvunjaji wa Masharti na Sera.

2.9 SHERIA 

Sera hizi za Huduma zinaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

2.10. TAARIFA NA MALALAMIKO

Taarifa zote na malalamiko kuhusiana na uvunjaji wa haki za haki zitawasilishwa kwa njia ya barua pepe au anwani ifuatayo.

 

 TAARIFA ZA WAZI:

      info@lughazetu.com  au

        Research and Development Network Ltd,

        C&G Plaza, 1st Floor, Mwai Kibaki Rd- Mikocheni

        S.L. P 7915, Dar es Salaam- Tanzania.  

 

MALAMIKO YA UKIUKAJI WA HAKI MILIKI NA LEBO ZA BIASHARA

        legal@lughazetu.com  

       au

       Research and Development Network Ltd,

       C&G Plaza, 1st Floor, Mwai Kibaki Rd- Mikocheni,  

       S. L. P 7915, Dar es Salaam- Tanzania.