Maswali na Majibu

1. Lugha Zetu ni nini?

Lugha Zetu ni huduma ya mtandao inayokuwezesha kujifunza na kuongea lugha. Huduma hii inaendeshwa na Kampuni ya Research and Development Network (RDN). Huduma yetu inakuwezesha kuzungumza lugha ya jamii au ya makabila ya Tanzania, lugha za Kitaifa, na Lugha za Afrika na za Kimataifa kwa urahisi na kwa haraka. Huduma hii, pia imetengenezwa kuhifadhi an kulinda lugha za Makabila ya Tanzania and Afrika kwa ujumla kama urithi na kuwezesha vijana kujifunza kwa urahisi.

 

2. Lugha gani naweza kujifunza katika tivuti ya Lughza Zetu

Unaweza kujifunza na kuongea Lugha za Makabila mbalimbali ya Tanzania, East Africa na Afrika kwa ujumla. Pia unaweza kujifunza lugha za Kitaifa za Afrika pamoja na lugha za Kimataifa kwenye tovuti yetu.

 

3. Kuna Lugha gapi kwa sasa ambazo naweza kujifunza na kuongea?

Kwa sasa, unaweza kujifunza na kuzungumza lugha zifuatazo: - Kiswahili, Kiingereza, Kisukuma, Kihaya, Kinyakyusa, Kipare, Kinyilamba, Kigogo, Kinyamwezi, Kimakonde, Kimaasai, Kihehe, Kichanga, Kinyaturu,...

                                 

4. Ninawezaje kupata huduma za Zetu Lugha?

Unaweza kupata huduma zetu kupitia tovuti yetu (www.lughazetu.com) kwa njia ya Kompyuta, na simu ya mkononi.

 

5. Kwa nini Lugha Zetu ni msaada wakati wa uhitaji wa kuongea lugha ingine?

Zetu Lugha ni msaidizi sana wakati wa mahitaji kwa sababu hauhitaji kukaa darasani na kupata mafunzo ili uweze kuzungumza lugha za watu wengine. Weka tu kipaza sauti chako, sikiliza na kisha uongee.

 

6. Kwa nini ni changue Lugha Zetu?

Lugha Zetu hutoa njia rahisi ya kuzungumza lugha za jamii ingine kwa urahisi na kwa haraka. Ni njia inayotumia tunza wakati na yenye ufanisi kwa sababu hauhitaji kuingia darasani au kusomea ili uweze kuzungumza. Unachotakiwa, Tumia dakika tano tu, jifunze maneno muhimu ambayo hutumiwa kwa jamii uliyotembelea, kisha ongea.

 

7. Je nahitaji akaunti ili niweze kutumia Lugha Zetu?

Ndiyo, lazima uwe na akaunti ili kutumia Lugha Zetu. Unaweza kujiandikisha au kuingia moja kwa moja kwenye tovuti yetu kwa kuweka jina lako na neno la siri. Pia unaweza kutumia akaunti yako ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, Google plus kujiunga au kuingia kwenye akaunti na kutumia huduma yetu. Kujiunga ni BURE. HAKUNA MALIPO.

 

8. Ninawezaje kuwasiliana na Lugha Zetu?

Wasiliana nasi kupitia:-

  • Email ya ofisi: support@lughazetu.com
  • Moja kwa moja kwenye mtandao: Msaada
  • Simu +255 222 781 294 na +255 782 412 822